14- Kufa katika njia ya kutetea mali inayotaka kuporwa. Kuhusu hilo kuna Hadiyth zifuatazo:
A- “Mwenye kuuawa kwa ajili ya mali yake.” [Katika upokezi mwingine imekuja: “Mwenye kutaka mali yake pasi na haki ambapo akapambana na akauliwa] basi huyo ni shahidi.”
Ameipokea al-Bukhaariy (05/93), Muslim (01/87), Abu Daawuud (02/285), an-Nasaa´iy (02/173) na at-Tirmidhiy (02/315). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Maajah (02/123), Ahmad (1668, 6823, 6829). Wote hawa wameipokea kwa upokezi wa pili isipokuwa tu al-Bukhaariy na Muslim ndio wamepokea kwa upokezi wa kwanza. Nao ni upokezi wa an-Nasaa´iy, at-Tirmidhiy na Ahmad (6822) wote kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr isipokuwa Ibn Maajah yeye kapokea kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar.
Kuhusiana na maudhui haya kumepokelewa Hadiyth kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd na itakuja katika alama ya kumi na tano.
B- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
“Kuna bwana mmoja alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Unaonaje akija mtu anataka kuichukua mali yangu?” Akamjibu: “Usimpe mali yako.” Akasema: “Unaonaje akinipiga vita?” Akamjibu: “Mpige vita.” Akamuuliza: “Unaonaje akiniua?” Akamjibu: “Wewe ni shahidi.” Akamuuliza: “Unaonaje nikimuua?” Akamjibu: “Yeye (ataingia) Motoni.”
Ameipokea Muslim (01/87), an-Nasaa´iy (02/173), Ahmad (01/339-360) ameipokea kwa njia nyingine kutoka kwake.
C- Mukhaariq (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:
“Kuna bwana mmoja alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Kuna mtu mmoja anakuja na kutaka mali yangu?” Akamjibu: “Mkumbushe juu ya Allaah.” Akasema: “Asipokumbushika?” Akamjibu: “Waombe msaada waislamu walioko pembezoni mwako dhidi yake.” Akasema: “Asipokuweko yeyote pembezoni mwangu katika waislamu?” Akamjibu: “Omba msaada kwa mtawala dhidi yake.” Akasema: “Vipi ikiwa mtawala atakuwa mbali nami” [anataka kuniwahi?”] Akamjibu: “Pambana kwa sababu ya mali yako mpaka uwe miongoni mwa mashahidi wa Aakhirah au mzuilie mali yako.”
Ameipokea an-Nasaa´iy na Ahmad (05/294, 294, 295) na ziada ni yake. Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh juu ya sharti za Muslim.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 56-57
- Imechapishwa: 11/02/2020

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 56-57
Imechapishwa: 11/02/2020
https://firqatunnajia.com/30-alama-za-mwisho-mwema-xvi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)