22. Kuipuuza dini ya Allaah kwa kutojifunza nayo wala kuitendea kazi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

10 – Kuipuuza dini ya Allaah (Ta´ala), hajifunzi nayo na wala haitendei kazi. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ

“Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayah za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi tutawalipiza wahalifu.”[1]

MAELEZO

Kichenguzi cha kumi: Kuipuuza dini ya Allaah kwa njia ya kwamba mtu akawa hajifunzi nayo na wala hamuabudu Allaah. Hiki ni kichenguzi miongoni mwa mambo yanayochengua Uislamu. Mwenye kukengeuka dini ya Allaah (´Azza wa Jall); hajifunzi nayo wala hamuabudu Allaah ni kafiri. Katika hali hii atakuwa ni mwenye kumuabudu shaytwaan. Haya ndio yale baadhi ya watu wanaita kuwa ni “mpagani”. Mtu asiyejifunza dini, hamuabudu Allaah na wala haitendei kazi. Huyu ni mwenye kumwabudu shaytwaan kwa sababu yeye ndiye ambaye amemuamrisha jambo hilo. Kwa hiyo huyu anakuwa ni mwenye kumuabudu shaytwaan. Hakuna yeyote duniani isipokuwa kuna anayemuabudu. Muabudu mzimu kuna wanachokiabudu. Mayahudi kuna wanachokiabudu. Manaswara kuna wanachokiabudu. Muislamu wanamwabudu Allaah. Asiyekuwa muislamu anamuabudu shaytwaan. Asiyemwabudu Allaah anamwabudu shaytwaan.

Huyu anayedai kuwa hajifunzi dini na hamuabudu Allaah anamtii shaytwaan na ni mja wa shaytwaan. Yeye ndiye ambaye amemuamrisha kufanya hilo na hivyo anakuwa ni mja wake. Mwenye kuipa mgongo dini ya Allaah akawa hajifunzi dini ya Allaah na wala hamuabudu Allaah kabisakabisa; si kwa kumuomba du´aa, swalah, mapenzi, maneno, kuamini pamoja na kuamini kuwa Allaah ndiye Muumbaji, Mruzukaji, Mwenye kuyaendesha mambo na kwamba Yeye ndiye muabudiwa wa haki, hajifunzi dini, kuamini wala haitakidi ya kwamba Allaah ndiye Muumbaji, Mruzukaji, Mwenye kuyaendesha mambo, kwamba Yeye ndiye mwenye kuabudiwa kwa haki, hajifunzi dini na wala hamwabudu Allaah, basi huyo ni kafiri. Ni kafiri kwa upuuzi wake. Kwa hiyo kile kitendo chenyewe cha kukengeuka ni ukafiri. Miongoni mwa dalili ya hilo ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ

“Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayah za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi tutawalipiza wahalifu.”[2]

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ

“Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyekumbushwa Aayah za Mola wake, akazipuuza na akayasahu yale iliyotanguliza mikono yake.”[3]

وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنذِرُوا مُعْرِضُونَ

“Na wale waliokufuru kwa yale wanayoonywa kwayo ni wenye kupuuza.”[4]

Makafiri wanakengeuka na kuyapuuza yale wanayoonywa ambayo ni kumuamini Allaah na Mtume Wake na kuitendea kazi dini hii. Amesema (Subhaanah):

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ

“Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayah za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi tutawalipiza wahalifu.”[1]

Kwa hivyo yule mwenye kuipuuza dini ya Allaah kwa njia ya kwamba akawa hajifunzi nayo na wala hamuabudu Allaah ni kafiri. Mtu kama huyu baadhi ya watu wanamwita kuwa ni mkanamungu na mpagani. Lakini uhalisia wa mambo ni kwamba anamwabudu shaytwaan. Hakuna asiyeabudu kitu. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa kuna anayemwabudu. Asiyemwabudu Allaah anamwabudu shaytwaan.

[1] 32:22

[2] 32:22

[3] 18:57

[4] 46:03

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 55-56
  • Imechapishwa: 15/04/2023