18. Ni lazima kwa mwanamke kubadilisha nguo zake akisafika na hedhi?


Swali 18: Ni lazima kwa mwanamke kuyabadilisha mavazi yake baada ya kusafika pamoja na kuzingatia kwamba hayakuingiwa na damu wala najisi?

Jibu: Hailazimu kufanya hivo. Hedhi haiunajisi mwili. Damu ya hedhi inanajisi kile ilichogusa peke yake. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaamrisha wanawake pindi mavazi yao yanapopatwa na damu ya hedhi basi wayaoshe na waswali ndani ya nguo zao hizo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 17
  • Imechapishwa: 27/06/2021