172. Mavazi ya eda yana rangi maalum?


Swali 172: Je, ni lazima kwa mwanamke aliyekaa eda kulazimiana na mavazi yenye rangi maalum kama wanavoashiria baadhi yao wanapomlazimu kuvaa nguo nyeupe ndani ya kile kipindi chote cha eda[1]?

Jibu: Haimlazimu mwanamke aliyekaa eda kuvaa mavazi maalum. Inafaa kwake kuvaa nguo nyeusi, nyeupe, kijani na manjano ambazo hazifanani na nguo za wanamme. Kinacholengwa ni kwamba avae nguo za wanawake ambazo hazifanani na nguo za wanamme. Lakini yasiwe ni mavazi ya mapampo na yenye kuvutia watu kumtazama.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/207).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 129
  • Imechapishwa: 29/01/2022