Inatakikana kwa mwanafunzi arudishe kila kitu kwa wenyewe. Haimstahikii mwanafunzi kuingia katika kila kitu. Utamuona kila kunapotokea kitu ameshakuwa msitari wa kwanza kukikimbilia na anapoteza wakati wake katika kitu hicho. Haina shaka ya kwamba hili ni kosa.

Mwanafunzi anatakiwa atambue kiwango chake, aiendee kazi yake na ajishughulishe na kile chenye kumnufaisha.

Ama kisichokuhusu na kinawahusu wanachuoni, Mashaykh na wakubwa awaachie wao.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016