16. Namna hii ndio baba atamchagulia mtoto jina zuri


Ni wajibu kwa baba kuchagua jina zuri lililobeba matamshi na maana nzuri kwa mujibu wa Shari´ah na lugha ya kiarabu. Jina linatakiwa liwe lizuri; linalotamkwa vizuri, zuri kulisikia. Linatakiwa kuwa na maana tukufu na nzuri na lisiwe na yale yote ambayo Shari´ah imeharamisha au kuchukiza kama vile majina yenye kutoka nje, linaloashiria ushabihisho na lililo na maana iliyojifunga.

Kwa msemo mwingine ni kwamba usichague jina isipokuwa baada ya kutafiti utamkaji na maana yake kupitia elimu, ufahamu na uelewa. Lililo salama zaidi ni kumtaka ushauri ambaye ni mjuzi. Kuna methali inayosema:

“Ni haki ya mtoto juu ya baba kumchagulia mama mzuri, kumpa jina nzuri na kumfunza adabu zilizokuwa nzuri.” Juu ya hilo kuna Hadiyth isiyokuwa Swahiyh[1].

[1] Tazama “as-Silsilah adh-Dhwa´iyfah” (199) na “Ittihaad-us-Saadah al-Muttaqiyn” (06/317-318).

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 18/03/2017