15. Hadiyth “Tofauti ya mwanachuoni ukimlinganisha na mfanya ´ibaadah… “

81- Kuna watu wawili walitajwa mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): mmoja ni mfanya ´ibaadah na mwengine ni mwanachuoni. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tofauti ya mwanachuoni ukimlinganisha na mfanya ´ibaadah ni kama tofauti kati yangu mimi na yule aliye chini kabisa kati yenu.”

Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Hakika Allaah, Malaika Wake na wakazi wa mbinguni na ardhini, mpaka waduduchungu ndani ya mashimo yao na nyangumi, wanamswalia yule ambaye anawafunza watu kheri.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy aliyesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/143)
  • Imechapishwa: 29/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy