143. Kuna du´aa maalum wakati wa kutoa mkono wa pole?


Swali 143: Baadhi ya watu wanapotaka kumliwaza mtu aliyefiwa na jamaa yao basi wanamwambia:

البقية في حياتك، وشد حيلك

Je, kuna kitu maalum kinachosemwa katika mnasaba kama huu? Je, ni lazima mtu afungamane nayo[1]?

Jibu: Sitambui du´aa maalum kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa yule anayetoa mkono wa pole ampe rambirambi ndugu yake kwa ajili ya Allaah juu ya mfiwa wao kwa maneno yanayofaa. Kwa mfano anaweza kusema:

جبر الله مصيبتك أحسن الله عزاءك وغفر لميتك

“Allaah aunge msiba wako, akufanye kuzuri kutaaziwa kwako na amsamehe maiti wako.”

Au mfano wa maneno kama hayo.

Kuhusu kutoa pole kwa kusema:

البقية في حياتك، وشد حيلك

sijui msingi wa maneno hayo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/380-381).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 21/01/2022