134. Uoanishi wa maandiko yanayohimiza Hijrah na yanayokataza


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا

“Enyi waja Wangu ambao mmeamini! Hakika ardhi Yangu ni pana, basi Mimi Pekee niabuduni.”[1]

al-Baghawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Sababu ya kuteremka Aayah hii kwa baadhi ya waislamu Makkah ambao hawakufanya Hijrah. Hivyo Allaah amewazungumzisha kwa jina la imani.”

MAELEZO

Aayah hii ni kutoka katika Suurah “al-´Ankabuut.” Ndani yake mna amri ya kuhajiri na kwamba ardhi ya Allaah ni pana. Ukiwa ndani ya nchi ambayo huwezi kuidhihirisha dini yako, basi tambua kuwa ardhi ya Allaah ni pana na unatakiwa kuhama kutoka hapo. Usibaki katika maeneo hayo mabaya. Bali toka ndani yake na kwenda katika ardhi ya Allaah pana. Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameipanua ardhi. Dalili ya kuhama kutoka katika Sunnah ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hijrah haitosimama mpaka Tawbah isimamishwe. Na Tawbah haitosimamishwa mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.”[2]

Kuhusu maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna Hijrah baada ya kufunguliwa [mji wa Makkah].”[3]

Udhahiri wa Hadiyth hii ni kwamba kuhama kumesita baada ya kufunguliwa mji wa Makkah. Baadhi ya watu wakafikiria kuwa kuna mgongano kati ya Hadiyth hii na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hijrah haitosimama mpaka Tawbah isimamishwe. Na Tawbah haitosimamishwa mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.”

Lakini wanachuoni wamejibu juu ya Hadiyth kwamba makusudio ya:

“Hakuna Hijrah baada ya kufunguliwa [mji wa Makkah].”

bi maana kutoka Makkah. Kwa sababu baada ya kufunguliwa umekuwa mji wa Kiislamu. Wanafikiria kuwa kuhama kumebaki kutoka Makkah baada ya kufunguliwa mji wa Makkah na hivyo wanataka kupata thawabu za Hijrah.

Kuhusu kuhama kutoka katika miji ya kikafiri ni jambo lenye kuendelea mpaka kusimame Qiyaamah. Dalili ya hilo ni zile Aayah zilizotangulia na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zilizotangulia. Haya ndio majibu juu ya utatizi huu.

[1] 29:59

[2] Abu Daawuud (3479), Ahmad (28/111) (16906).

[3] al-Bukhaariy (2783) na Muslim (1353) (85)  kabla ya Hadiyth ya (1864) (86) kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambayo ameipokea Muslim (1864) kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 268-270
  • Imechapishwa: 11/02/2021