Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba kutoa jina kunapitika katika nyakati tatu:

1- Mtoto anapewa jina siku ile ile anayozaliwa.

2- Zile siku tatu za kwanza baada ya kuzaliwa.

3- Siku ya saba baada ya kuzaliwa.

Tofauti hii ina maana ya kwamba yote ni sawa na himdi zote zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 14
  • Imechapishwa: 18/03/2017