112. Hivi ndivo inafahamika Hadiyth ya ´Aaishah

Swali 112: Ni vipi itafasiriwa Hadiyth ya mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumfunza ´Aaishah du´aa ya kuyatembelea makaburi[1]?

Jibu: Kuyatembelea makaburi mwanzoni ilikuwa imekatazwa kwa watu wote. Baadaye wakaruhusiwa watu wote. Kisha baadaye ikawa makatazo ni maalum kwa wanawake tu. Kujengea juu ya haya mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumfunza ´Aiashah adabu ya matembezi yalitokea katika kipindi ambapo matembezi ki-Shari´ahh yanakubalika kwa wote.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/331).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 84
  • Imechapishwa: 09/01/2022