Punde umejua kutoka katika maneno ya wanazuoni ya kwamba hakukuthibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kitu chochote juu ya ubora wa usiku wa ijumaa ya kwanza ya Rajab wala ubora wa usiku wa nusu ya Sha´baan. Ndipo ikatambulika kuwa kusherehekea mambo hayo ni Bid´ah iliyozuliwa katika Uislamu. Vivyo hivyo kuufanya maalum kwa chochote katika ´ibaadah ni Bid´ah iliokemewa. Vivyo hivyo usiku wa tarehe 27 Rajab – ambao ndio wanaitakidi baadhi ya watu kuwa ni usiku wa Israa´ na Mi´raaj – haifai kuufanya maalum kwa kufanya chochote katika ´ibaadah kama ambavo haijuzu kuusherehekea. Hayo ni kutokana na dalili zilizotangulia. Hapa ni pale ambapo kutajulikana. Tusemeje ikiwa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni ni kwamba usiku huo hautambuliki. Maneno ya waliosema kuwa ni usiku wa tarehe 27 Rajab ni maneno ya batili na hayana msingi wowote katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Amefanya vizuri yule aliyesema:

Uzuri wa mambo ni yale yaliyotangulia juu ya uongofu

Uovu wa mambo ni yale ya kizushi yaliyozuliwa

Swalah na amani zimwendee mja na Mtume Wake; Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 33
  • Imechapishwa: 19/01/2022