692- Halafu akapokea kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh kutoka kwa Ibn ´Abbaas aliyesema:

“Nilimwambia Ibn ´Abbaas: “Wanadai kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ogeni siku ya ijumaa, osheni vichwa vyenu hata kama hamna janaba na wala hamkujitia manukato.”

Ibn ´Abbaas akasema:

“Kuhusu manukato sijui, lakini ni kweli kuhusiana na kuoga.”[1]

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com