1. Utangulizi wa “al-Fusuul fiy Siraat-ir-Rasuul”

Himdi zote ni za Allaah. Salaam kwa wale aliowateua. Himdi zilizokuwa nyingi, nzuri na zenye baraka kama jinsi anavyopenda Mola Wetu na kuridhia. Ninashuhudia ya kwamba hapana mola wa haki isipokuwa Allaah Pekee, hali ya kuwa hana mshirika. Allaah amsifu na amsalimu Mtume Wake mwaminifu na kiumbe Chake bora Muhammad mpaka siku ya Qiyaamah na awawie radhi Maswahabah zake, wake zake, kizazi chake na kila mwandamizi aliye na busara.

Amma ba´d:

Sio jambo lenye kupendeza kwa wanachuoni kupuuzia zama za ulinganizi wa kitume na historia ya Kiislamu kwa vile iko na elimu kubwa na faida muhimu ambayo mwanachuoni hawezi kujitosheleza nayo na wala hapewi udhuru wa kukosa kuijua.

Hivyo nimependa kuandika kuhusu hilo kwa njia ya ukumbusho ili kufungua njia ya maudhi hii na kuweka msingi na na kuchangia mchango juu yake. Ninamtegemea Allaah na kumwachia kila kitu Yeye. Ukumbusho huo ndani yake mna nasabu ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maisha na sifa zake pamoja na zama za Uislamu baada ya kufa kwake mpaka leo hii. Watu wenye busara ni wenye haja kubwa nayo. Ukumbusho utakuwa kwa njia ya ufupisho – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 7-8
  • Imechapishwa: 18/03/2017