Swali: Hivi sasa kuna propaganda zinazoendelea katika baadhi ya vyombo vya mawasiliano zinazolingania kufanya upya utamkaji wa kidini. Unasemaje juu ya hilo na ni yepi malengo yao?

Jibu: Utamkaji wa kidini ndio uliotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Watu wanatakiwa kuitwa kama walivyoitwa humo; kafiri anatakiwa kuitwa kafiri (كافر), mnafiki anatakiwa kuitwa mnafiki (منافق), fasiki anatakiwa kuitwa fasiki (فاسق), muumini anatakiwa kuitwa muumini (مؤمن). Hili ni jambo la lazima.

Ama kuyabadili majina haya na mtu akasema haitakiwi kusema kafiri na badala yake mtu aseme “asiye muislamu”, huku ni kuyapotosha maneno, kuwaridhisha makafiri na kupakana mafuta katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Ikiwa malengo ni kuyabadili yale matamshi yaliyotajwa katika Qur-aan na Sunnah, haijuzu. Kuna khatari kubwa. Ni kupotosha. Ikiwa malengo ni ule usulubu wa mtoa mawaidha au mlinganizi, inatofautiana kutegemea na watu. Awazungumzishe kwa ile njia inayowaathiri na kuwafaa. Usulubu na maneno ya mlinganizi yanatofautiana. Wafalme hawazungumzishwi kama wanavyozungumzishwa watu wa kawaida. Wanachuoni hawazungumzishwi kama wanavyozungumzishwa wajinga. Inategemea. Kila mmoja anatakiwa kuzungumzishwa kwa namna inayolingana naye.

Ikiwa malengo ni yule mlinganizi anayelingania, anayemrisha mema na kukataza maovu na kwamba anatakiwa kuzungumza kwa namna inayostahiki, hili linatakiwa kudhibitiwa. Ama ikiwa malengo ni yale majina na zile hukumu zilizoko katika Qur-aan na Sunnah, haijuzu kuyabadilisha kwa hali yoyote ile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5436
  • Imechapishwa: 17/03/2017