09. Kinga ya tisa ya janga la corona: Kusimama usiku kuswali

9- Kusimama usiku kuswali

Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Lazimianeni na kusimama usiku kuswali. Hakika ndivo walivokuwa wakifanya wema kabla yenu. Kusimama usiku kuswali na kumkurubia Allaah, kunamlinda mtu kutokamana na madhambi, kunafuta makosa na kunaondosha magonjwa mwilini.”[1]

[1] at-Tirmidhiy na wengineo.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 12
  • Imechapishwa: 05/04/2020