10. Kinga ya kumi ya janga la corona: Kufunika vyombo na machupa ya maji

10- Kufunika vyombo na machupa ya maji

Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Funikeni vyombo na viriba vya maji. Hakika kwa mwaka kuna usiku ambapo kunashuka janga; halipiti kwenye chombo kisichokuwa na mfuniko wala kiriba cha maji kilicho wazi isipokuwa linashuka ndani yavyo.”[1]

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni kitu ambacho madaktari hawana elimu nacho.”[2]

[1] Muslim.

[2] Zaad-ul-Ma´aad.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 13
  • Imechapishwa: 05/04/2020