09. Hadiyth “Wale ambao hawakufunga leo wameenda na thawabu… “

1061- Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika safari. Miongoni mwetu wako waliokuwa wamefunga na wengine hawakufunga. Tukapiga kambi katika siku ya joto. Wengi wetu waliokuwa wamefanyiwa kivuli ni watu wa kitambara. Miongoni mwetu wako waliokuwa wakizuia jua kwa mikono yao. Wakaanguka chini wafungaji na ambao hawafunga wakasimama na kuanza kujenga vibanda na kuwapa maji vipando vya wanyama. Ndipo Mtume wa Alllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wale ambao hawakufunga leo wameenda na thawabu.”[1]

Ameipokea Muslim[2].

[1] Swahiyh.

[2] Pia al-Bukhaariy, an-Nasaa’iy na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/617)
  • Imechapishwa: 22/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy