Shaykh Bakr amesema:

“Nimetazama nikaona kuwa kitabu hiki kinakosa tafiti za misingi ya kielimu, kutopendelea kielimu, mfumo wa ukosoaji wa sawa, uaminifu wa unukuaji na wa elimu na uadilifu. Kuhusu adabu za mazungumzo, usulubu wa uandikaji na hadhi ya utafiti, haiwezi hata kufikiriwa.”

Ametakasika Allaah kutokamana na mapungufu. Yote aliyosema Shaykh Bakr yanapatikana katika maneno yake mwenyewe haya. Pamoja na kuwa ni maneno machache tu, yana kasoro zenye kutia aibu zinazokosa tafiti za misingi ya kielimu, kupinda kutoka katika mfumo wa haki, ukosefu wa uaminifu wa unukuaji na wa elimu na kuikataa haki. Kuhusu adabu za mazungumzo, ziko mbali kabisa iwezekanavyo katika maneno haya. Huenda hakulifikiria hilo. Ama usulubu wa uandikaji na hadhi ya utafiti, unaweza kuwauliza wenye busara na inswafu kuhusu vitabu vyangu. Namshukuru Allaah kuona vitabu vyangu vinapendwa na wenye kupenda haki. Vinawafurahisha waumini na vinawakasirisha watu wa batili. Ni vya kipekee vilivyo na tafiti nzuri, uandishi wenye nguvu na usulubu mzuri wa uandishi na dalili na hoja zenye nguvu na havina maneno ya ubunifu na ya kigeni ambayo wajinga wanadhani kuwa ni balagha kwa vile uhalisia wa mambo si waweza.