06 – Shaykh Bakr anachelea Qutwub asije kupata matendo mema ya al-Madkhaliy

Umedai:

“Sipendelei mimi na waislamu wengine wote kutumbukia kwenye madhambi. Hakika ni katika dhuluma mbaya kwa mtu kuyatoa matendo yake mema kumpa mtu ambaye ana chuki na uadui kwake.”

Ametakasika Allaah. Unakusudia nini kwa kusema hivi?

Hivi kweli unataka kufunga aina moja wapo kubwa ya Jihaad na kuitetea haki na Sunnah kwa sababu ya Sayyid Qutwub?

Unaonelea kuwa matendo yangu mema yanaenda kwa Sayyid Qutwub nikiweka bidii katika kuwatetea Maswahabah, kuraddi ujamaa wake, kughadhibika kwa kutukanywa Nabii wa Allaah Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuponda tafasiri zake za kimakosa za batili? Wewe umeshaanza kutubia kwa kumraddi Abu Ghuddah na as-Swaabuuniy? Umefikia ya kwamba Ruduud zako ina maana ni kuwazawadia matendo yako mema? Kama mambo ni hivyo basi sote madhambi yetu yako namna hiyo, nako ni kwa kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah.