06. Wafunge vipi wale ambao michana au nyusiku zao zinakuwa ima ndefu sana au fupi sana?

Swali 06: Kipi wafanye wale ambao mchana wao unakuwa kwa masaa ishirini na moja? Je, wakadirie yale masaa ya funga? Kipi wafanye wale ambao mchana wao unakuwa mfupi sana? Kadhalika ambao mchana wao unaendelea kwa miezi sita na usiku wao unaendelea kwa miezi sita?

Jibu: Wale ambao wana usiku na mchana kwa muda wa masaa ishirini na nne basi wanatakiwa kufunga katika kile kipindi cha mchana. Ni mamoja mchana ukawa mfupi au mrefu. Hayo yatawatosha na himdi zote njema anastahiki Allaah. Haijalishi kitu hata kama mchana wao ni mfupi. Ama kuhusu wale ambao mchana na usiku wao unaendelea kama mfano miezi sita basi wanatakiwa kukadiria swawm na swalah viwango vyake, kama alivyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika siku ya ad-Dajjaal ambayo itakuwa ni kama mwaka, vivyo hivyo ile siku ambayo itakuwa kama mwezi na wiki. Basi watatakiwa kukadiria swalah kiwango chake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 09
  • Imechapishwa: 10/04/2019