Vitenguzi vya Uislamu na ukafiri wa mwenye kuacha swalah

Swali: Miongoni mwa mambo yaliyokuwa mashuhuri kwa Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ni kwamba vichenguzi vya Uislamu ni kumi. Ni kwa nini alikomeka juu ya idadi hii[1]? Ni katika kichenguzi kipi anaingia mwenye kuacha swalah?

Jibu: Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) alipotaja vitenguzi vya Uislamu kwamba ni kumi haikuwa kwa njia ya ukomo. Bali ni kwa njia ya mfano. Kwa msemo mwingine maana yake ni kwamba miongoni mwa vitenguzi vya Uislamu ni pamoja na hivi kumi.

Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) aliishi katika wakati ambapo kulikuwa na shirki. Ndipo akataja vitenguzi vya Uislamu kwa kuzingatia wakati wake hali ya kuwatahadharisha watu juu ya vitenguzi hivi.

Kuhusu mwenye kuacha swalah, Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Maswahabah ambayo yamenukuliwa na zaidi ya mmoja, vyote ni vyenye kufahamisha dalili ya kwamba mwenye kuacha swalah ni kafiri. Haijalishi kitu hata kama atafanya hivo kwa uvivu.

[1] https://firqatunnajia.com/hakuna-vitenguzi-isipokuwa-tu-vile-kumi-alivyotaja-imaam-ibn-abdil-wahhaab/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (48) http://binothaimeen.net/content/1109
  • Imechapishwa: 10/04/2019