05. Kinga ya tano ya janga la corona: Kuomba kusalimishwa asubuhi na jioni

5- Kumuomba Allaah usalama asubuhi na jioni

´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa haziachi du´aa hizi wakati anapoamka asubuhi na wakati anapoingiliwa na jioni:

اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا والآخِرَةِ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ والْعَافِيَةَ في دِيني ودُنْيَايَ وأَهْلِي وَمَالِي اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي وآمِنْ رَوْعَاتِي اللَّهُمَّ احْفَظنِي بَيْنَ يَدَيَّ وَمِنْ خَلْفِي وَعَنْ يَمِيني وَعَنْ شِمَالِي وَمِنْ فَوْقِي وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba usalama duniani na Aakhirah. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba msamaha na afya katika dini, dunia yangu, familia yangu na mali yangu. Ee Allaah! Nifichie aibu zangu na ziaminishe tisho zangu. Ee Allaah! Nilinde mbele yangu, nyuma yangu, kulianu kwangu, kushotoni kwangu na juu yangu. Najilinda kwa utukufu Wako kuuliwa chini yangu.”[1]

[1] Ahmad na wengineo.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 9
  • Imechapishwa: 01/04/2020