05. Hakuna dalili ya kwamba asiyeswali ni muislamu

Hakuna si katika Qur-aan wala Sunnah ya kwamba asiyeswali sio kafiri au ya kwamba ni muumini. Kubwa lililothibiti juu ya maudhui hii ni dalili zinazoonyesha fadhila na thawabu za Tawhiyd na kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Dalili hizi ima zimefungamanishwa na mambo yenye kuzuia kuacha swalah au vilevile zimetajwa katika hali maalum ambapo mtu anapewa udhuru kwa kutokuswali. Zinaweza vilevile kuwa kijumla. Katika hali hiyo zinatakiwa kufasiriwa kwa dalili zinazothibitisha kuwa asiyeswali ni kafiri. Dalili zinazoonyesha kuwa asiyeswali ni kafiri ni maalum na ambazo ni maalum zinatangulia kabla ya ambazo ni jumla.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 8
  • Imechapishwa: 22/10/2016