6- Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kheri hii ni hazina na hazina hiyo iko na funguo zake. Twuubaa kwa mja ambaye Allaah amemfanya kuwa ni ufunguo wa kheri na kufungwa kwa shari. Na maangamivu kwa yule mja ambaye Allaah amemfanya kuwa ni ufunguo wa shari na kufungwa kwa kheri.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah na tamko ni lake na Ibn Abiy ´Aaswim. Cheni ya wapokezi ina ulaini.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/135)
  • Imechapishwa: 29/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy