05. Dalili ya nne kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

4- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mja anapotoa swadaqah ya kitu kizuri, basi Allaah huipokea na huishika kwa mkono Wake wa kuume na kuielea, kama anavyolea mmoja wenu kitekli chake, mpaka inakuwa kama Uhud. Pindi mmoja wenu anapotoa tonge la chakula basi linalelewa mikononi mwa Allaah mpaka linakuwa kama Uhud. Hivyo toeni swadaqah!”[1]

Hadiyth hizi ni Swahiyh.

[1] ´Abdur-Razzaaq (20050).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 11/12/2018