03. Hadiyth “Si katika wema kufunga safarini… “

1055- ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulirudi kutoka vitani pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tulisafiri katika siku yenye joto kali. Tukapiga kambi katika baadhi ya njia ambapo bwana mmoja katika sisi akaondoka na kujiweka chini ya mti. Marafiki zake wakamzunguka wakati ambapo alikuwa amelala akihisi machungu. Pindi Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaona akasema: “Ana nini mwenzenu?” Wakasema: “Amefunga.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Si katika wema kufunga safarini. Lazimianeni na ruhusa ya Allaah ambayo amekupeni na muikubali.”[1]

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/615)
  • Imechapishwa: 22/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy