فإن العبادة : اسم جامع لكل ما يحبه الله ويرضاه من الأقوال والأعمال الباطنة والظاهرة
ومنها الدعاء، وقد قال تعالى

´Ibaadah ni kila neno na kitendo, cha dhahiri na kilichojificha, ambacho Allaah anakipenda na kukiridhia. Mfano wa ´ibaadah ni kama du´aa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Mahala pa kuswalia kote ni kwa ajili ya Allaah; basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.”[1]

والدليل على أن دعوة غير الله كفر، كما قال تعالى

Dalili ya kwamba kumuomba asiyekuwa Allaah ni kufuru ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Na yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hawafaulu makafiri.”[2]

وذلك أن الدعاء من أعظم أنواع العبادات، كما قال ربكم

Hili ni kwa sababu du´aa ni moja katika aina kubwa za ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ

“Na Mola wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na ‘ibaadah Yangu basi wataingia Motoni hali ya kudhalilika.”[3]

وفي (السنن): عن أنس مرفوعاً

Katika vitabu vya Sunan imepokelewa kupitia kwa Anas ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

الدعاء مخ العبادة

“Du´aa ndio kiini cha ´ibaadah.”[4]

[1] 72:18

[2] 23:117

[3] 40:60

[4] at-Tirmidhiy (3371). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf-ul-Jaami´” (3003).

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 12-15