أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

بسم الله الرحمن الرحيم

Himdi zote ni za Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salaam zimwendee kiongozi wa Mitume, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Amma ba´d:

Hiki ni kijitabu chenye manufaa ambacho ni wajibu kwa mtu kumfunza nacho mtoto kabla ya kujifunza Qur-aan. Lengo ni ili wawe waislamu wakamilifu kutokamana na maumbile ya Kiislamu na wamuabudu Allaah peke yake kutokamana na imani. Nimepangilia kitabu hiki kwa njia ya maswali na majibu:’

إذا قيل لك : من ربك

Swali 1: Ni nani Mola wako?

فقل : ربي الله

Jibu: Mola wangu ni Allaah.

وما معنى الرب

Swali 2: Ni nini maana ya “Mola”?

فقل : المالك المعبود والمعين … الله … ذو الألوهية والعبودية على خلقه أجمعين

Jibu: Maana yake ni “Mmiliki na muabudiwa”. Maana ya Allaah ni “Yule mwenye kuabudiwa na viumbe wote”.

فإذا قيل لك : بما عرفت ربك؟

Swali 3: Umemjuaje Mola wako?

فقل : أعرفه بآياته ومخلوقاته، ومن آياته: الليل والنهار، والشمس والقمر

Jibu: Nimemtambua kwa alama na viumbe Vyake. Miongoni mwa alama Zake ni usiku na mchana, jua na mwezi.

ومن مخلوقاته: السموات والأرض، وما فيهما، والدليل على ذلك قوله تعالى

Miongoni mwa viumbe Vyake ni mbingu, ardhi na vilivyomo ndani yake. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Hakika Mola wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha Akalingana juu ya ´Arshi. Anafunika usiku kwa mchana – unaufuatia upesi upesi na [Ameumba] jua na mwezi na nyota [vyote] vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Ni Vyake Pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

فإن قيل لك: لأي شيء خلقك؟

Swali 4: Ni kwa nini amekuumba?

فقل : لعبادته وحده لا شريك له، وطاعته بمثال ما أمر به، وترك ما ينهى عنه، كما قال الله تعالى

Jibu: Kwa ajili ya kumuabudu Yeye peke yake na kutomshirikisha na yeyote na kumtii kwa kutekeleza yale Aliyoamrisha na kujiepusha na yale Aliyokataza. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Na Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.”[2]

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

“Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.”

Shirki ndio dhambi kubwa ambayo Allaah kaasiwa nayo. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ

“Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni.”[3]

والشرك : أن يجعل لله نداً يدعوه، ويرجوه، أو يخافه، أو يتوكل عليه، أو يرغب إليه من دون الله، وغير ذلك من أنواع العبادات

Shirki ni kumfanyia Allaah mwenza kwa njia ya kwamba akawa anaombwa, kutarajiwa, kutegemewa au akawa anatamaniwa badala ya Allaah.

[1] 07:54

[2] 51:56

[3] 05:72

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 2-7
  • Imechapishwa: 25/03/2017