02. Hadiyth “Mtume wa Allaah alikuwa anapotoa Khutbah… “

50- Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapotoa Khutbah basi macho yake yanapiga wekundu, sauti yake inapaa na ghadhabu zake zinakuwa kali. Ni kana kwamba analitahadharisha jeshi na husema: “Asubuhi na jioni yenu!”[1] Akisema: “Nimetumilizwa mimi na Qiyaamah kama viliw hivi”, anaambatanisha kidole cha shahada na cha kidole kirefu. Kisha anasema: Amma ba´d: Hakika maneno bora ni Kitabu cha Allaah na uongofu bora ni uongofu wa Muhammad. Uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa. Kila kilichozuliwa ni Bid´ah. Kila Bid´ah ni upotevu.” Kisha anasema: ”Mimi nina haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake mwenyewe. Yule mwenye kuacha mali ni kwa ajili ya familia yake. Na atakayeacha deni basi ulipaji wake uko juu yangu na yule atakayeacha mali iko kwa warithi wake.”[2]

Ameipokea Muslim, Ibn Maajah na wengineo.

[1] Adui amekuteremkieni asubuhi.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/128)
  • Imechapishwa: 27/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy