49- ´Aiaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayezusha katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud kwa tamko lisemalo:

“Yule atakayefanya kitu kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”

Ameipokea Ibn Maajah. Katika upokezi wa Muslim imekuja:

“Yule atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/128)
  • Imechapishwa: 27/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy