Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na salamu zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake, Maswahabah na wale waliowafuata kwa uongofu wao.

Amma ba´d:

Nimesoma yale yaliyoenezwa na gazeti la al-Madiynah tarehe 10 Rabiy´ al-Aakhir 1403 namba 5785 ambayo yalikuwa ni majibu yaliotolewa kuwajibu baadhi ya waandishi juu ya maswali ya jarida la Luviva Romavsin. Baadhi niliyokuta ndani yake ni yafuatayo:

“Mzozo kati ya unaswara na Uislamu, jambo ambalo mimi mwenyewe nimelikashifu. Nimegundua kwamba baadhi ya wamishonari wa kikristo wanaeneza vipeperushi katika ulimwengu wa tatu vinavyoukosoa Uislamu. Vivyo hivyo najua pia baadhi ya wahubiri wa Kiislamu wanachapisha na kueneza vitabu vinavyokosoa unaswara. Mambo haya yananisikitisha sana. Uislamu na unaswara ni dini mbili zilizoteremshwa. Sisi sote tunamwamini mungu mmoja. Kwa ajili hiyo ni lazima kwetu tuepuke mizozo aina yote kati ya dini hizo mbili na tufanye kuwe na mapatano kati ya waislamu na manaswara katika kumtumikia mwanadamu.”

Kutokana na makosa ya wazi na yasiyokuwa wazi yaliyomo ndani ya maneno haya ndipo ikawa ni lazima kwangu na kwa watu mfano wangu kuzindua makosa yaliyotokea katika maneno haya yanayokwenda kinyume na Shari´ah safi. Nasema:

Mzozo kati ya Uislamu na dini nyenginezo kukiwemo uyahudi, unaswara, budha na nyenginezo ni jambo lililokuwa endelevu tangu hapo Allaah alipomtumiliza Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka hii leo. Uislamu unawasema vibaya mayahudi na manaswara na kuwatia kasoro kwa matendo yao mabaya na unasema waziwazi kwamba ni makafiri kwa lengo la kuwatahadharisha waislamu kutokamana nao. Amesema (Ta´ala):

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا

”Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa waliyoyasema.”[1]

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ

”Mkono wa Allaah umefumbwa.” [Sivyo hivyo, bali] mikono yao ndio ilivyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema na kuua kwao Manabii pasi na haki.”[2]

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ

”Hakika wamekufuru wale ambao wamesema: “Hakika Allaah ni al-Masiyh mwana wa Maryam.”[3]

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.””[4]

Zipo Aayah nyingi zinazowasema vibaya mayahudi na manaswara na kutahadharisha ule upotofu waliyomo. Amesema kuhusu washirikina wengine kama mabudha na wengineo:

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini na mjakazi muumini ni bora kuliko mshirikina ijapo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe [wanawake wa Kiislamu] wanaume washirikina mpaka waamini na mtumwa muumini ni bora kuliko mshirikina ijapo akikupendezeni – hao wanaitia katika Moto na Allaah anaitia katika Pepo na msamaha kwa idhini Yake na anabainisha Aayah Zake ili wapate kukumbuka.”[5]

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَاۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ

“Hakika wale waliokufuru ambao ni watu wa kitabu na washirikina watakuwa ndani ya Moto wa Jahannam hali ya kudumu humo – hao ndio waovu kabisa wa viumbe.”[6]

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

”Yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[7]

Zipo Aayah nyingi zenye maana kama hii.

Imesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Laana ya Allaah iwe juu ya mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu ya kuswalia.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea namna ambavo Umm Habiybah na Ummah Salamah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) walimtajia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kanisa waliloona Uhabeshi na namna ilivyokuwa na mapicha. Akasema:

“Hao ndio wale ambao wanapofiwa na mtu mwema au mja mwema, basi hujenga juu ya kaburi lake msikiti na huchora ndani yake picha hiyo. Hao ndio viumbe waovu kabisa mbele ya Allaah.”

Zipo Hadiyth nyingi zenye maana kama hii.

[1] 05:64

[2] 03:181

[3] 05:17

[4] 05:73

[5] 02:221

[6] 98:06

[7] 03:85

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 05/10/2021