105- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kujifunza elimu katika yale ambayo kwayo kunakusudiwa uso wa Allaah (Ta´ala) na hajifunzi isipokuwa ni kwa lengo la kupata jambo la kidunia, basi hatopata harufu ya Pepo siku ya Qiyaamah.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Haakim aliyesema:

“Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/153)
  • Imechapishwa: 02/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy