714- ´Abdullaah bin Busr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anatoa Khutbah siku ya ijumaa alikuja mtu mmoja akijipenyeza kati ya watu. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Keti chini. Hakika umeudhi na umechelewa.”[1]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” yake na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” yake. Si kwa Abu Daawuud wala kwa an-Nasaa’iy hakuna tamko lisemalo ”… na umechelewa.”. Kwa Ibn Khuzaymah imekuja:

”Hakika umeudhi na umeudhiwa.”[2]

715- Amipokea Ibn Maajah kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah[3].

[1] Swahiyh.

[2] Mimi nachelea kwamba ima yeye au mchapa kitabu ameandika makosa kwenye nuskha. Kilichothibiti kutoka katika chapa yake (3/156/1811) kinaafikiana na upokezi wa Ahmad (4/190) kilichojengeka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy na akafuatwa na Ibn Wahb kwa Ibn-ul-Jaarud katika ”al-Muntaqaa” (110/294) na Ibn Hibbaan (572).

[3] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/446)
  • Imechapishwa: 08/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy