Swali: Nina mali niliyoikusanya kutokana na mshahara wangu wa kila mwezi kwa muda wa mwaka. Je, inayo zakaah ilhali siweki tarehe maalum ya kuitumia?
Jibu: Ikiwa mfanyakazi anaweka akiba kutoka katika mshahara wake, basi anatakiwa kuirekodi kwa kuandika ili ajue mwanzo wake na mwisho wake. Kila unapokamilika mwaka juu ya kiasi fulani, atatoa zakaah yake ya robo ya kumi (1/40). Ikiwa anaweka akiba kila mwezi 1,000 au 2,000, basi aandike mwezi alioweka akiba. Inapokamilika mwaka juu yake, basi atazitolea zakaah. Vivyo hivyo mwezi wa pili, mwezi wa tatu na kila mwezi anatoa zakaah unapofikisha mwaka wake. Ikiwa atatoa zakaah ya yote mara moja pale unapokamilika mwaka wa mwezi wa kwanza, basi inajuzu na zakaah ya miezi iliyofuata itahesabika kuwa imelipwa mapema na hilo halina madhara.
Muulizaji: Kwa maana kila mwezi anatoa zakaah yake?
Ibn Baaz: Kila mwezi inapokamilika mwaka wake, inakuwa wajibu kutoa zakaah, kisha mwezi wa pili vivyo hivyo, mwezi wa tatu, wa nne na kuendelea.
Mwanafunzi: Kwa maan§a ni kama analipa zakaah kila mwezi?
Ibn Baaz: Ndiyo.
Mwanafunzi: Kwa msingi kwamba kila mwezi umepitia miezi kumi na miwili?
Ibn Baaz: Ndivyo hivyo. Ikiwa atatoa zakaah ya yote mwanzo wa mwaka mmoja, basi kusudio linapatikana na miezi iliyochelewa zakaah yake itahesabiwa tayari imelipwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3205/زكاة-الراتب-الشهري
- Imechapishwa: 25/10/2026
Swali: Nina mali niliyoikusanya kutokana na mshahara wangu wa kila mwezi kwa muda wa mwaka. Je, inayo zakaah ilhali siweki tarehe maalum ya kuitumia?
Jibu: Ikiwa mfanyakazi anaweka akiba kutoka katika mshahara wake, basi anatakiwa kuirekodi kwa kuandika ili ajue mwanzo wake na mwisho wake. Kila unapokamilika mwaka juu ya kiasi fulani, atatoa zakaah yake ya robo ya kumi (1/40). Ikiwa anaweka akiba kila mwezi 1,000 au 2,000, basi aandike mwezi alioweka akiba. Inapokamilika mwaka juu yake, basi atazitolea zakaah. Vivyo hivyo mwezi wa pili, mwezi wa tatu na kila mwezi anatoa zakaah unapofikisha mwaka wake. Ikiwa atatoa zakaah ya yote mara moja pale unapokamilika mwaka wa mwezi wa kwanza, basi inajuzu na zakaah ya miezi iliyofuata itahesabika kuwa imelipwa mapema na hilo halina madhara.
Muulizaji: Kwa maana kila mwezi anatoa zakaah yake?
Ibn Baaz: Kila mwezi inapokamilika mwaka wake, inakuwa wajibu kutoa zakaah, kisha mwezi wa pili vivyo hivyo, mwezi wa tatu, wa nne na kuendelea.
Mwanafunzi: Kwa maan§a ni kama analipa zakaah kila mwezi?
Ibn Baaz: Ndiyo.
Mwanafunzi: Kwa msingi kwamba kila mwezi umepitia miezi kumi na miwili?
Ibn Baaz: Ndivyo hivyo. Ikiwa atatoa zakaah ya yote mwanzo wa mwaka mmoja, basi kusudio linapatikana na miezi iliyochelewa zakaah yake itahesabiwa tayari imelipwa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3205/زكاة-الراتب-الشهري
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-ya-mshahara-wa-kila-mwezi/