Swali: Amenijia mgeni nyumbani kwangu. Je, inajuzu nimwache ndani ya nyumba yangu katika chumba chake peke yake huku mke wangu akiwa chumba chake au jikoni au hili linahesabika kuwa ni mwanaume na mwanamke kukaa faragha?
Jibu: Haijuzu kuwaacha wawili hao peke yao. Bali ni lazima ubaki pamoja na mgeni au utoke pamoja naye ikiwa hakuna mtu mwingine nyumbani isipokuwa mke wako peke yake. Ama ikiwa pamoja na mke wako kuna mwanamke mwingine, basi hakuna ubaya. Lakini ikiwa yuko peke yake, basi hafai kubaki na mgeni. Kwa sababu mgeni si lazima awe ni mtu wa kuaminika; huenda akawa mbaya au huenda amekuja kwa makusudi mabaya. Hivyo ni lazima kujihadhari. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kukaa faragha na akasema:
“Asiwe mwanaume peke yake na mwanamke, kwani hakika shaytwaan huwa ni wa tatu wao.”
Hivyo haifai kumwacha mke wako pamoja na mgeni. Bali mtoke pamoja au mkae pamoja mpaka Allaah aondoe hali hiyo.
Swali: Vipi ikiwa mgeni yuko katika chumba chake na mke yuko katika chumba chake?
Jibu: Hata hivyo ni kosa, muda wa kuwa anajua kuwa hakuna mtu mwingine nyumbani.
Swali: Mfano mtu amepata mgeni ghafla ambapo akatoka kwenda dukani kununua mkate au kitu cha kumhudumia mgeni, inaweza kuonekana kama anamtilia shaka au kumtia aibu?
Jibu: Inawezekana, lakini anaweza kumleta jirani au mwanamke mwingine akae na mke wake au kufanya jitihada yoyote itakayozuia khatari kadiri iwezekanavyo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3176/حكم-ترك-الضيف-في-المنزل-من-دون-محرم
- Imechapishwa: 25/10/2026
Swali: Amenijia mgeni nyumbani kwangu. Je, inajuzu nimwache ndani ya nyumba yangu katika chumba chake peke yake huku mke wangu akiwa chumba chake au jikoni au hili linahesabika kuwa ni mwanaume na mwanamke kukaa faragha?
Jibu: Haijuzu kuwaacha wawili hao peke yao. Bali ni lazima ubaki pamoja na mgeni au utoke pamoja naye ikiwa hakuna mtu mwingine nyumbani isipokuwa mke wako peke yake. Ama ikiwa pamoja na mke wako kuna mwanamke mwingine, basi hakuna ubaya. Lakini ikiwa yuko peke yake, basi hafai kubaki na mgeni. Kwa sababu mgeni si lazima awe ni mtu wa kuaminika; huenda akawa mbaya au huenda amekuja kwa makusudi mabaya. Hivyo ni lazima kujihadhari. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kukaa faragha na akasema:
“Asiwe mwanaume peke yake na mwanamke, kwani hakika shaytwaan huwa ni wa tatu wao.”
Hivyo haifai kumwacha mke wako pamoja na mgeni. Bali mtoke pamoja au mkae pamoja mpaka Allaah aondoe hali hiyo.
Swali: Vipi ikiwa mgeni yuko katika chumba chake na mke yuko katika chumba chake?
Jibu: Hata hivyo ni kosa, muda wa kuwa anajua kuwa hakuna mtu mwingine nyumbani.
Swali: Mfano mtu amepata mgeni ghafla ambapo akatoka kwenda dukani kununua mkate au kitu cha kumhudumia mgeni, inaweza kuonekana kama anamtilia shaka au kumtia aibu?
Jibu: Inawezekana, lakini anaweza kumleta jirani au mwanamke mwingine akae na mke wake au kufanya jitihada yoyote itakayozuia khatari kadiri iwezekanavyo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3176/حكم-ترك-الضيف-في-المنزل-من-دون-محرم
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/kumwacha-mgeni-wa-kiume-nyumbani-pamoja-na-mke-wangu/