Swali: Imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza mauzo mawili ndani ya mauzo moja. Ni ipi picha yake na ni ipi sababu ya kuharamishwa kwake?
Jibu: Bora zaidi lililosemwa katika hilo ni kwamba mauzo mawili ndani ya mauzo moja ni (بيعة العينة), kwa maana kuuza kwa kuunganisha mikataba miwili katika mkataba mmoja. Kwa msemo mwingine kuweka sharti la mkataba ndani ya mkataba mwingine. Kwa ajili hiyo imepokelewa katika Hadiyth Swahiyh:
“Atakayefanya mauzo mawili ndani ya mauzo moja, basi atapata iliyo pungufu kati ya viwili au ribaa.”
Hii inaelezea kwamba maana ya “mauzo mawili ndani ya mauzo moja” (بيعة العينة), nayo ni kwamba mtu anauza bidhaa kwa mtu kwa mfano kwa 100 kwa malipo ya kucheleweshwa, kisha anaichukua tena kutoka kwake kwa pesa 70 au 80 taslimu. Hivyo haya ni mauzo mawili ndani ya mauzo moja, wamefanya hila ya kufikia ribaa. Anampa sabini taslimu na baadaye atachukua 100 baada ya miezi au baada ya mwaka. Haya ni mauzo mawili ndani ya mauzo moja, basi atastahiki ile iliyo pungufu, yaani 70 aliyotoa na hataruhusiwa kuchukua ziada. Bali anarudishiwa tu alichotoa. Hili ndilo linaloitwa (بيعة العينة); kwa namna kwamba anachukua pesa taslimu kwa deni, anasema bidhaa hii ninakuuzia kwa 1,000 mpaka Ramadhaan ijayo, kisha anainunua tena kwa bei ya haraka ya 700 au 800 ili apate fedha ya matumizi yake. Maana yake ni kwamba amechukua 700 au 800 kwa deni la 1,000 iliyocheleweshwa, jambo ambalo ndio ribaa yenyewe.
Miongoni mwa picha nyingine, kama walivyotaja wanazuoni, ni kununua bidhaa kwa sharti kwamba atamuuzia bidhaa nyingine, kwa sharti kwamba atamkopesha kiasi fulani au atamkodisha kitu fulani. Kwa mfano ananunua gari kwa 10,000 kwa sharti kwamba amuuzie nyumba yake kwa 20,000, ananunua nyumba yake kwa sharti kwamba amuuzie ardhi yake fulani kwa kiasi fulani au kwa sharti kwamba amkopeshe kiasi fulani cha mali. Huu ni mkataba ndani ya mkataba. Huu ndio unaoitwa mauzo mawili ndani ya mauzo moja.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3207/صورة-البيعتين-في-بيعة-وعلة-التحريم-في-ذلك
- Imechapishwa: 25/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3207/صورة-البيعتين-في-بيعة-وعلة-التحريم-في-ذلك
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/picha-za-mauzo-mawili-ndani-ya-uzo-moja/