Zakaah ni faradhi kwa kila muislamu aliye huru na mwenye kumiliki kikamilifu kile kiwango ambacho kinawajibisha kutoa zakaah. Hakuna zakaah katika mali mpaka ipite juu yake mwaka mmoja, isipokuwa mazao yanayotoka ardhini na ongezeko la kiwango cha zakaah kutokana na uzao na faida; kwani mwaka wao ni mwaka wa asili yao.
Zakaah hailazimiki isipokuwa katika aina nne:
1 – Wanyama wa mifugo wanaolishwa malishoni.
2 – Mazao yanayotoka ardhini.
3 – Sarafu.
4 – Bidhaa za biashara.
Hakuna zakaah katika chochote kati ya hivyo mpaka kifikie kile kiwango ambacho kinawajibisha kutoa zakaah. Zakaah inawajibika katika ziada ya kiwango cha zakaah kwa hesabu yake. Isipokuwa wanyama wa mifugo wanaolishwa malishoni; hakuna chochote katika mali ya ziada inayolipwa iliyo baina ya vile viwango viwili vya zakaah.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 34
- Imechapishwa: 25/10/2026
Zakaah ni faradhi kwa kila muislamu aliye huru na mwenye kumiliki kikamilifu kile kiwango ambacho kinawajibisha kutoa zakaah. Hakuna zakaah katika mali mpaka ipite juu yake mwaka mmoja, isipokuwa mazao yanayotoka ardhini na ongezeko la kiwango cha zakaah kutokana na uzao na faida; kwani mwaka wao ni mwaka wa asili yao.
Zakaah hailazimiki isipokuwa katika aina nne:
1 – Wanyama wa mifugo wanaolishwa malishoni.
2 – Mazao yanayotoka ardhini.
3 – Sarafu.
4 – Bidhaa za biashara.
Hakuna zakaah katika chochote kati ya hivyo mpaka kifikie kile kiwango ambacho kinawajibisha kutoa zakaah. Zakaah inawajibika katika ziada ya kiwango cha zakaah kwa hesabu yake. Isipokuwa wanyama wa mifugo wanaolishwa malishoni; hakuna chochote katika mali ya ziada inayolipwa iliyo baina ya vile viwango viwili vya zakaah.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 34
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/37-zakaah-na-hukumu-yake/