36. Mkono wa pole na matembezi ya kaburi

Inapendeza kumzika maiti ndani ya mwanandani. Huwekwa juu yake matofali kwa kusimamishwa, kama ilivyofanywa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuingizwi ndani ya kaburi tofali zilizookwa, wala mbao, wala kitu chochote kilichoguswa na moto.

Inapendeza kuwapa pole watu wa maiti. Kulia juu yake si jambo lenye kuchukiza ikiwa hakufuatani na malalamiko wala maombolezo.

Hapana vibaya kwa wanaume kuyatembelea makaburi. Anapopita karibu nayo au anapoyatembelea atasema:

سلام عليكم أَهْلَ  دار قوم مؤمنين، وإنا إِنْ شَاءَ اللهُ بكم لاحقون، اللهم لا تحرمنا أجرهم ولا تفتنا بعدهم و اغفر لنا و لهم  نَسْأَلُ الله لَنَا وَلَكُمْ الْعَافِية

“Amani iwe juu yenu, enyi watu wa makazi ya watu waumini! Hakika sisi –  Allaah akitaka – tutajiunga nanyi. Ee Allaah! Usitunyime ujira wao, wala usitutie katika mtihani baada yao na utusamehe sisi na wao. Tunamuomba Allaah atupe sisi na nyinyi afya na usalama.”[1]

´Ibaadah yoyote ya kujikurubisha kwa Allaah ambayo mtu ataifanya na akafanya thawabu zake kuwa za maiti muislamu, basi itamnufaisha.

[1] Ibn Maajah (1546), Ahmad (8/102) na Abu Ya´laa (8/97). al-Albaaniy amesema:

“Dhaifu. Imetajwa katika “Irwaa’-ul-Ghaliyl” (3/237) na “ar-Rawdhw an-Nadhiyr” (775). Imesihi isipokuwa tu jumla isemayo:

اللهم لا تحرمنا أجرهم ولا تفتنا بعدهم

”Ee Allaah! Usitunyime ujira wao, wala usitutie katika mtihani baada yao.”

Ndio maana nimeitaja pia katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (1266).” (Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah (302)

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 34
  • Imechapishwa: 25/10/2026