Ikiwa imeshindikana kumuosha maiti kwa sababu ya kutokuwepo kwa maji au kwa kuogopa mwili wake kukatika vipande, kama mwenye ugonjwa wa kuambukiza au aliyeungua, au kwa kuwa mwanamke yuko miongoni mwa wanaume au mwanamume yuko miongoni mwa wanawake, basi hufanyishwa Tayammum. Isipokuwa kwamba kila mmoja kati ya wanandoa wawili anaweza kumuosha mwenzake. Vivyo hivyo kijakazi ambaye amezaa na mmiliki wake anaweza kumuosha bwana wake.
Shahidi anapokufa katika uwanja wa vita, haoshwi na wala haswaliwi. Huvuliwa chuma na ngozi alizovaa, kisha hufunikwa ndani ya nguo zake. Hata hivyo hapana vibaya ikiwa atavikwa sanda kwa nguo nyingine.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 34
- Imechapishwa: 25/10/2026
Ikiwa imeshindikana kumuosha maiti kwa sababu ya kutokuwepo kwa maji au kwa kuogopa mwili wake kukatika vipande, kama mwenye ugonjwa wa kuambukiza au aliyeungua, au kwa kuwa mwanamke yuko miongoni mwa wanaume au mwanamume yuko miongoni mwa wanawake, basi hufanyishwa Tayammum. Isipokuwa kwamba kila mmoja kati ya wanandoa wawili anaweza kumuosha mwenzake. Vivyo hivyo kijakazi ambaye amezaa na mmiliki wake anaweza kumuosha bwana wake.
Shahidi anapokufa katika uwanja wa vita, haoshwi na wala haswaliwi. Huvuliwa chuma na ngozi alizovaa, kisha hufunikwa ndani ya nguo zake. Hata hivyo hapana vibaya ikiwa atavikwa sanda kwa nguo nyingine.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 34
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/35-maiti-aliyeshindikana-kuoshwa/