Swali: Muulizaji anauliza kuhusu kuchangia pesa katika ardhi na zimepita juu yake miaka kadhaa. Je, inapaswa kutolewa zakaah?

Jibu: Ikiwa alichangia kwa nia ya biashara, ya kuuza na kununua, basi kuna zakaah juu yake kwa miaka iliyopita, robo ya kumi, katika thamani yake. Kila mwaka inapimwa thamani yake, kila mwaka kwa kiwango inachostahili na anatolea zakaah ya robo ya kumi ikiwa ardhi ni ya kuuza na kununua kwa biashara.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1461/حكم-زكاة-الارض-المعدة-للتجارة
  • Imechapishwa: 20/12/2025