Zakaah kwa wafanyakazi wenye mishahara midogo

Swali: Wafanyakazi wanaokuja huku mishahara yao ni midogo na maisha yao ni ya kutosheleza tu maisha na wana watoto wadhaifu. Je, inajuzu kuwapa zakaah?

Jibu: Iwapo wametambulika kuwa wanahitaji na kwamba mishahara yao haikidhi mahitaji yao na ni waislamu wanaojulikana hivyo, basi hakuna ubaya kuwapa sehemu ya zakaah ili kuziba haja. Ikiwa wametambulika kuwa ni waislamu na wametambulika kwa ukweli na kwamba wao ni wahitaji mafakiri, kwa sababu watu wengi hudai ufakiri na ni waongo ilihali mishahara yao inawatosheleza. Ikiwa wametambulika kwa uhitaji kwa ukweli na akashuhudia mtu anayeaminika kuwa ni fakiri na kwamba mshahara wake ni mdogo na mchache, hautoshelezi mahitaji yake, basi hakuna ubaya kumpa. Vinginevyo hapewi, bali watafutwe watu wanaojulikana kuwa wahitaji na waislamu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1061/هل-تحل-الزكاة-على-الوافدين-لضعف-رواتبهم
  • Imechapishwa: 13/01/2026