Swali: Je, inajuzu kutoa zakaah kwa ajili ya ujenzi wa misikiti? Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ

“… na katika njia ya Allaah.”[1]

Jibu: Tayari tumeshataja ya kwamba makusudio ya Aayah hiyo ni wapiganaji katika jihaad. Kwa maana nyingine ni wale wanaopigana katika njia ya Allaah. Kwa hiyo zakaah haitolewi katika ujenzi wa misikiti wala katika shule. Hilo ni kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi. Maoni sahihi miongoni mwa wanazuoni – na ndio ambayo ni maafikiano yao – ni kwamba zakaah inapaswa kutolewa tu katika makundi yale manane yaliyotajwa wazi na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Misikiti na shule hazipo katika makundi hayo. Maana ya Aayah jihaad na wale wanaopigana katika njia hiyo. Baadhi ya wanazuoni wa hivi karibuni wameruhusu kuitumia katika miradi ya kheri. Hata hivyo ni maoni dhaifu kwa sababu yanakwenda kinyume na dalili za Kishari’ah na kinyume na njia iliyofuatwa na wanazuoni wa mwanzo katika masuala ya zakaah.

[1] 09:60

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1063/هل-تصرف-الزكاة-في-بناء-المساجد
  • Imechapishwa: 23/01/2026