Swali: Je, inajuzu kwa mtu kutoa katika zakaah ya mali yake kwa ajili ya kujenga msikiti uliokaribia kukamilika na ujenzi wake ukasimama?

Jibu: Linalojulikana kwa wanazuoni wote na maoni ya wanazuoni wengi ni kwamba – nayo ndio maafikiano ya wanazuoni ya Salaf wema wa mwanzo – ni kwamba zakaah haitolewi katika kujenga misikiti, kununua vitabu na mfano wa hayo. Bali hutolewa kwa makundi manane: mafakiri, masikini, wanaoikusanya, wanaolainishwa nyoyo zao, katika kuwakomboa watumwa, wenye deni, katika njia ya Allaah na msafiri aliyeharibikiwa. Kilicho katika njia ya Allaah kinakusudiwa Jihaad. Hili ndilo linalojulikana kwa wanazuoni. Si miongoni mwa hayo kuitoa katika kujenga misikiti, kujenga shule, barabara wala mfano wa hayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/982/هل-يشرع-بناء-المساجد-من-زكاة-المال
  • Imechapishwa: 24/12/2025