Swali: Ni ipi hukumu ya zakaah juu ya hazina iliyofukuliwa?
Jibu: Ikiwa hazina hiyo ni mpya basi kinazingatiwa ni cha mwokotaji. Katika hali hiyo atatakiwa kukitangaza kwa muda wa mwaka mzima. Akipata mmiliki ni vyema na vyenginevyo atabaki nacho yeye. Na ikiwa hazina hiyo ni ya zamani kwa namna ya kwamba dhana kubwa inapelekea kwamba si cha yeyote anayetambulika katika wale watu wanaoeshi katika kipindi hicho, ni cha yule mwokotaji. Hata hivyo atalazimika kutoa sehemu moja ya tano yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hazina iliyochimbuliwa itatolewa sehemu moja ya tano yake.”[1]
[1] al-Bukhaariy (1499) na Muslim (1710).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/88)
- Imechapishwa: 23/05/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya zakaah juu ya hazina iliyofukuliwa?
Jibu: Ikiwa hazina hiyo ni mpya basi kinazingatiwa ni cha mwokotaji. Katika hali hiyo atatakiwa kukitangaza kwa muda wa mwaka mzima. Akipata mmiliki ni vyema na vyenginevyo atabaki nacho yeye. Na ikiwa hazina hiyo ni ya zamani kwa namna ya kwamba dhana kubwa inapelekea kwamba si cha yeyote anayetambulika katika wale watu wanaoeshi katika kipindi hicho, ni cha yule mwokotaji. Hata hivyo atalazimika kutoa sehemu moja ya tano yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hazina iliyochimbuliwa itatolewa sehemu moja ya tano yake.”[1]
[1] al-Bukhaariy (1499) na Muslim (1710).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/88)
Imechapishwa: 23/05/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-juu-ya-hazina-iliyofukuliwa/