Swali: Je, inafaa kupunguza pua kubwa kwa kufanya upasuaji wa plastiki?
Jibu: Kanuni juu ya suala hili ni kwamba upasuaji kwa ajili ya kuondoa kasoro inafaa na upasuaji kwa ajili ya kujipamba haijuzu. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wanaotia mwanya kwa ajili ya kuyapamba meno yao. Upande mwingine alimpa idhini Swahabah wakati ilipokatwa pua yake katika vita kuweka pua kuweka pua bandia ya dhahabu. Kwa hivyo kanuni ni kwamba upasuaji wa plastiki kwa ajili ya kuondoa kasoro inafaa na ambayo ni kwa ajili ya kuzidisha urembo haijuzu. Kwa mfano yule ambaye pua yake imepinda na akafanya operesheni kwa ajili ya kuirekebisha, kwa sababu huko ni kuondoa kasoro. Vivyo hivyo ni sawa kwa yule ambaye yuko na kengeza. Ikiwa mtu pua yake kubwa kunazingatiwa kuwa ni kasoro, basi hapana vibaya kufanya upasuaji. Lakini ikiwa pua hiyo ni ndogo na operesheni inapelekea kuifanya nzuri zaidi, basi huko kunazingatiwa ni kama kutia mwanya – na kutia mwanya hakujuzu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/49-50)
- Imechapishwa: 23/05/2026
Swali: Je, inafaa kupunguza pua kubwa kwa kufanya upasuaji wa plastiki?
Jibu: Kanuni juu ya suala hili ni kwamba upasuaji kwa ajili ya kuondoa kasoro inafaa na upasuaji kwa ajili ya kujipamba haijuzu. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wanaotia mwanya kwa ajili ya kuyapamba meno yao. Upande mwingine alimpa idhini Swahabah wakati ilipokatwa pua yake katika vita kuweka pua kuweka pua bandia ya dhahabu. Kwa hivyo kanuni ni kwamba upasuaji wa plastiki kwa ajili ya kuondoa kasoro inafaa na ambayo ni kwa ajili ya kuzidisha urembo haijuzu. Kwa mfano yule ambaye pua yake imepinda na akafanya operesheni kwa ajili ya kuirekebisha, kwa sababu huko ni kuondoa kasoro. Vivyo hivyo ni sawa kwa yule ambaye yuko na kengeza. Ikiwa mtu pua yake kubwa kunazingatiwa kuwa ni kasoro, basi hapana vibaya kufanya upasuaji. Lakini ikiwa pua hiyo ni ndogo na operesheni inapelekea kuifanya nzuri zaidi, basi huko kunazingatiwa ni kama kutia mwanya – na kutia mwanya hakujuzu.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/49-50)
Imechapishwa: 23/05/2026
https://firqatunnajia.com/operesheni-ya-pua-kubwa/