Abu Bakr bin Abiy Shaybah amesimulia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye alikuwa haoni ubaya wa kuyasomea maji kisha kummwagia nayo mgonjwa[1].
Katika kitabu hichohicho imekuja ya kwamba Swaalih bin Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahumaa Allaah) amesema:
“Wakati mwingine nakuwa mgonjwa baba yangu akichukua kikombe cha maji na kusoma juu yake. Halafu ananiamrisha niyanywe na kuyaosha uso na mikono yangu.”[2]
Siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja kwa Thaabit bin Qays (Radhiya Allaahu ´anh) akiwa mgonjwa akamwambia:
“Ee Mola wa watu! Ondoa ungonjwa kutoka kwa Thaabit bin Qays bin Shammaas!” Kisha alichukua mchanga kutoka Butwhaan, kisha akauweka ndani ya chombo kisha akaweka maji na kusoma na akammwagia nayo.”[3]
[1] al-Aadaab ash-Shar´iyyah (3/103-104).
[2] al-Aadaab ash-Shar´iyyah (3/477).
[3] Abu Daawuud (3885). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3885).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/38)
- Imechapishwa: 23/05/2026
Abu Bakr bin Abiy Shaybah amesimulia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye alikuwa haoni ubaya wa kuyasomea maji kisha kummwagia nayo mgonjwa[1].
Katika kitabu hichohicho imekuja ya kwamba Swaalih bin Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahumaa Allaah) amesema:
“Wakati mwingine nakuwa mgonjwa baba yangu akichukua kikombe cha maji na kusoma juu yake. Halafu ananiamrisha niyanywe na kuyaosha uso na mikono yangu.”[2]
Siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja kwa Thaabit bin Qays (Radhiya Allaahu ´anh) akiwa mgonjwa akamwambia:
“Ee Mola wa watu! Ondoa ungonjwa kutoka kwa Thaabit bin Qays bin Shammaas!” Kisha alichukua mchanga kutoka Butwhaan, kisha akauweka ndani ya chombo kisha akaweka maji na kusoma na akammwagia nayo.”[3]
[1] al-Aadaab ash-Shar´iyyah (3/103-104).
[2] al-Aadaab ash-Shar´iyyah (3/477).
[3] Abu Daawuud (3885). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3885).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/38)
Imechapishwa: 23/05/2026
https://firqatunnajia.com/matabano-na-maji/