Adhaana wakati wa kulipa swalah

Swali: Je, ni wajibu kutoa adhaana juu ya swalah anayokidhi mtu?

Jibu: Ikiwa kundi la watu wanaishi ndani ya mji ambapo kumeshaadhiniwa ambapo wakapitiwa na usingizi na wakaamka baada ya kuchomoza kwa jua, basi sio wajibu kwao kutoa adhaana. Kwa sababu ile adhaana ya jumla ya ndani ya mji inatosheleza na inadondosha ile faradhi. Lakini ikiwa wako mahali ambapo hakuadhiniwi, basi ni wajibu kutoa adhaana. Wakati siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) safarini alipochukuliwa na usingizi kutokana na Fajr na akaamka baada ya kuchomoza kwa jua, alimwamrisha Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh) kuadhini na kukimu. Hili linajulisha kuwa ni wajibu. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utapofika wakati wa swalah, basi aadhini mmoja wenu na mkubwa wenu aswalishe.”[1]

Hadiyth ni yenye kuenea na inahusu ndani na nje ya wakati.

[1] al-Bukhaariy (628).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/163)
  • Imechapishwa: 23/05/2026