Namna ya mgonjwa kukidhi swalah nyingi zilizompita

Swali: Kuna mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji na akapitwa na swalah nyingi za faradhi. Je, ataziswali kwa pamoja baada ya kupona kwake au aziswali kila kipindi cha swalah pamoja na wakati wake; kwa mfano Dhuhr wakati wa Dhuhr na kadhalika?

Jibu: Ni lazima kwake aziswali zote kwa pamoja katika wakati mmoja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) alipopitwa na ´Aswr katika vita vya Khandaq aliiswali kabla ya Maghrib. Kwa hiyo ni lazima kwa mtu pale anapokosa baadhi ya swalah za faradhi aziswali kwa pamoja na azicheleweshe.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/223)
  • Imechapishwa: 22/05/2026