Swali: Nilikuwa na 5000 SAR mfukoni mwangu za kutoa zakaah. Nilikuwa nataka kuwapa wenye kuistahiki lakini hata hivyo ikanipotea au nikaibiwa kabla ya kuitoa. Je, ni lazima kuitoa kwa mara nyingine?

Jibu: Hukuitoa mpaka useme kuwa ni kwa mara nyingine. Ni lazima kwako kuitoa. Kwa sababu haikuwafikia wenye kuistahiki. Dhimma yako haijatakasika mpaka iwafikie wenye kuistahiki. Vingnevyo bado iko katika dhimma yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (17) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtf-08011435.mp3
  • Imechapishwa: 18/10/2019